Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 5:17-27 Biblia Habari Njema (BHN)

17. “Heri mtu yule ambaye Mungu anamrudi!Hivyo usidharau Mungu Mwenye Nguvu anapokuadhibu.

18. Kwani yeye huumiza na pia huuguza;hujeruhi, na kwa mkono wake huponya.

19. Atakuokoa katika maafa zaidi ya mara moja;katika balaa la mwisho, uovu hautakugusa.

20. Wakati wa njaa atakuokoa na kifo,katika mapigano makali atakuokoa.

21. Utakingwa salama na mashambulio ya ulimi,wala hutaogopa maangamizi yajapo.

22. Maangamizi na njaa vijapo, utacheka,wala hutawaogopa wanyama wakali wa nchi.

23. Nawe utaafikiana na mawe ya shambani,na wanyama wakali watakuwa na amani nawe.

24. Utaona nyumbani mwako mna usalama;utakagua mifugo yako utaiona yote ipo.

25. Utaona pia wazawa wako watakuwa wengi,wengi kama nyasi mashambani.

26. Utafariki ukiwa mkongwe mtimilifu,kama mganda wa ngano ya kupurwa iliyoiva vizuri.

27. Basi huu ndio utafiti wetu; tena ni ukweli;uusikie na kuuelewa kwa faida yako.”

Kusoma sura kamili Yobu 5