Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 5:1-10 Biblia Habari Njema (BHN)

1. “Ita sasa, uone kama kuna wa kukuitikia.Ni yupi kati ya watakatifu utakayemwita?

2. Ama kweli hangaiko humuua mpumbavu,na wivu humwangamiza mjinga.

3. Nimepata kuona mpumbavu akifana,lakini ghafla nikayalaani makao yake.

4. Watoto wake hawana usalama;hudhulumiwa mahakamani,na hakuna mtu wa kuwatetea.

5. Mazao yake huliwa na wenye njaa,hata nafaka iliyoota kati ya miiba;wenye tamaa huuonea shauku utajiri wake.

6. Kwa kawaida mateso hayatoki mavumbiniwala matatizo hayachipui udongoni.

7. Bali binadamu huzaliwa apate taabu,kama cheche za moto zirukavyo juu.

8. “Kama ningekuwa wewe ningemgeukia Mungu,ningemwekea yeye Mungu kisa changu,

9. yeye atendaye makuu yasiyochunguzika,atendaye maajabu yasiyohesabika.

10. Huinyeshea nchi mvua,hupeleka maji mashambani.

Kusoma sura kamili Yobu 5