Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 42:13-17 Biblia Habari Njema (BHN)

13. Alikuwa pia na watoto wa kiume saba na wa kike watatu.

14. Binti yake wa kwanza alimpa jina Yemima, wa pili Kezia, na wa mwisho Keren-hapuki.

15. Katika nchi yote hiyo hapakuwa na wanawake waliokuwa wazuri kama mabinti wa Yobu. Baba yao akawaachia urithi kama alivyowaachia kaka zao.

16. Baada ya hapo, Yobu aliishi miaka 140, akawaona wajukuu na vitukuu vyake vyote hadi kizazi cha nne.

17. Basi, Yobu akafariki akiwa mzee wa miaka mingi.

Kusoma sura kamili Yobu 42