Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 40:1-13 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Mwenyezi-Mungu akaendelea kumwambia Yobu:

2. “Je, wewe mwenye kuchunguza makosa utashindana na Mungu Mwenye Nguvu?Wewe unayebishana nami Mungu, basi jibu mambo hayo!”

3. Kisha Yobu akamjibu Mwenyezi-Mungu:

4. “Mimi sifai kitu nitakujibu nini?Naufunga mdomo wangu.

5. Nilithubutu kusema na sitasema tena.Nilisisitiza lakini sitaendelea kusema zaidi.”

6. Hapo Mwenyezi-Mungu akamjibu kutoka kimbunga:

7. “Jikaze kama mwanamume.Nitakuuliza, nawe utanijibu.

8. Je, unataka kweli kubatilisha hukumu yangu,kuniona nina hatia ili wewe usiwe na hatia?

9. Je, una nguvu kama mimi Mungu?Waweza kunguruma kwa sauti kama yangu?

10. “Basi, jioneshe kuwa na fahari na ukuu,ujipambe kwa utukufu na fahari.

11. Wamwagie watu hasira yako kuu;mwangalie kila mwenye kiburi na kumwangusha.

12. Mwangalie kila mwenye kiburi na kumporomosha,uwakanyage waovu mahali walipo.

13. Wazike wote pamoja ardhini;mfunge kila mmoja kwa kifungo cha kifo.

Kusoma sura kamili Yobu 40