Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 4:1-6 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Kisha Elifazi yule Mtemani akamjibu Yobu:

2. “Je, mtu akijaribu kukuambia neno utakasirika?Lakini nani awezaye kujizuia kusema?

3. Sikiliza! Wewe umewafundisha wengi,na kuiimarisha mikono ya wanyonge.

4. Maneno yako yamewainua waliokufa moyo,umewaimarisha waliokosa nguvu.

5. Lakini sasa yamekupata, nawe ukakosa subira,yamekugusa, nawe ukafadhaika.

6. Je, kumcha Mungu si ndilo tegemeo lako?Na unyofu wako si ndilo tumaini lako?

Kusoma sura kamili Yobu 4