Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 39:9-17 Biblia Habari Njema (BHN)

9. “Je, nyati atakubali kukutumikia?Au je, atakubali kulala zizini mwako?

10. Je, waweza kumfunga nyati kamba kulima shamba,au avute jembe la kulimia?

11. Je, utamtegemea kwa kuwa ana nguvu nyingina kumwacha akufanyie kazi zako nzito?

12. Je, wamtazamia nyati akuvunie mavuno yako,na kuleta nafaka mahali pa kupuria?

13. “Mbuni hupigapiga mabawa yake kwa madaha,lakini hawezi kuruka kama korongo.

14. Mbuni huyaacha mayai yake juu ya ardhiili yapate joto mchangani;

15. lakini hajui kama yanaweza kukanyagwa,au kuvunjwa na mnyama wa porini.

16. Mbuni huwatendea wanawe ukatili kama si wake,hata kazi yake ikiharibika yeye hana wasiwasi;

17. kwa sababu nilimfanya asahau hekima yake,wala sikumpa sehemu yoyote ya akili.

Kusoma sura kamili Yobu 39