Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 39:5-12 Biblia Habari Njema (BHN)

5. “Nani aliyemwacha huru pundamwitu?Nani aliyewaacha waende kwa kuwafungua?

6. Mimi niliwapa jangwa liwe makao yao,mbuga zenye chumvi kuwa makazi yao.

7. Hujitenga kabisa na makelele ya miji,hasikilizi kelele ya kumfanyisha kazi.

8. Hutembeatembea milimani kupata malisho,na kutafuta chochote kilicho kibichi.

9. “Je, nyati atakubali kukutumikia?Au je, atakubali kulala zizini mwako?

10. Je, waweza kumfunga nyati kamba kulima shamba,au avute jembe la kulimia?

11. Je, utamtegemea kwa kuwa ana nguvu nyingina kumwacha akufanyie kazi zako nzito?

12. Je, wamtazamia nyati akuvunie mavuno yako,na kuleta nafaka mahali pa kupuria?

Kusoma sura kamili Yobu 39