Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 39:24-30 Biblia Habari Njema (BHN)

24. Farasi husonga mbele, akitetemeka kwa hasira;tarumbeta iliapo, yeye hasimami.

25. Kila ipigwapo tarumbeta, yeye hutoa sauti;huisikia harufu ya vita toka mbali,huusikia mshindo wa makamandawakitoa amri kwa makelele.

26. “Je, mwewe amejifunza kwako jinsi ya kuruka,na kunyosha mabawa yake kuelekea kusini?

27. Je, tai hupaa juu kwa amri yako,na kuweka kiota chake juu milimani?

28. Tai hufanya makazi yake juu ya miamba mirefu,na ncha kali za majabali ndizo ngome zake.

29. Kutoka huko huotea mawindo,macho yake huyaona kutoka mbali.

30. Makinda yake hufyonza damu;pale ulipo mzoga ndipo alipo tai.”

Kusoma sura kamili Yobu 39