Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 39:22-27 Biblia Habari Njema (BHN)

22. Farasi huicheka hofu, na hatishiki;wala upanga hauwezi kumrudisha nyuma.

23. Silaha wachukuazo wapandafarasi,hugongana kwa sauti na kungaa juani.

24. Farasi husonga mbele, akitetemeka kwa hasira;tarumbeta iliapo, yeye hasimami.

25. Kila ipigwapo tarumbeta, yeye hutoa sauti;huisikia harufu ya vita toka mbali,huusikia mshindo wa makamandawakitoa amri kwa makelele.

26. “Je, mwewe amejifunza kwako jinsi ya kuruka,na kunyosha mabawa yake kuelekea kusini?

27. Je, tai hupaa juu kwa amri yako,na kuweka kiota chake juu milimani?

Kusoma sura kamili Yobu 39