Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 37:9-17 Biblia Habari Njema (BHN)

9. Dhoruba huvuma kutoka chumba chake,na baridi kali kutoka ghalani mwake.

10. Kwa pumzi ya Mungu barafu hutokea,uso wa maji huganda kwa haraka.

11. Mungu hulijaza wingu manyunyu mazito;mawingu husambaza umeme wake.

12. Kwa amri yake vyote huzunguka huku na huko,kutekeleza kila kitu anachokiamuru,kufanyika katika ulimwengu wa viumbe.

13. Mungu hutekeleza matakwa yake duniani;iwe ni kwa ajili ya kuwaadhibu watu,au kwa ajili ya kuonesha upendo wake.

14. “Unapaswa kusikiliza Yobu;nyamaza, usikilize maajabu ya Mungu.

15. Je, wajua jinsi Mungu anavyovipa amri yake,na kufanya umeme wa mawingu yake ungae?

16. Je, wajua jinsi mawingu yanavyoelea angani?Ndizo kazi za ajabu za yule aliye mkamilifu wa maarifa!

17. Wewe wajiona umevaa nguo za joto sana,wakati upepo wa kusi unaivamia nchi.

Kusoma sura kamili Yobu 37