Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 37:1-11 Biblia Habari Njema (BHN)

1. “Kutokana na hayo, moyo wangu unatetemeka,na kuruka kutoka mahali pake.

2. Sikilizeni ngurumo ya sauti ya Mungu,na mvumo wa sauti kutoka kinywani mwake.

3. Huufanya uenee chini ya mbingu yote,umeme wake huueneza pembe zote za dunia.

4. Ndipo sauti yake hunguruma,sauti ya Mungu hunguruma kwa faharina muda huo wote umeme humulikamulika.

5. Mungu hupiga radi ya ajabu kwa sauti yake,hufanya mambo makuu tusiyoweza kuyaelewa.

6. Huiambia theluji, ‘Anguka juu ya nchi!’Na manyunyu na mvua, ‘Nyesha kwa nguvu.’

7. Hufunga shughuli za kila mtu;ili watu wote watambue kazi yake.

8. Wanyama wa porini hurudi mafichoni mwao,na hubaki katika mapango yao.

9. Dhoruba huvuma kutoka chumba chake,na baridi kali kutoka ghalani mwake.

10. Kwa pumzi ya Mungu barafu hutokea,uso wa maji huganda kwa haraka.

11. Mungu hulijaza wingu manyunyu mazito;mawingu husambaza umeme wake.

Kusoma sura kamili Yobu 37