Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 36:24-33 Biblia Habari Njema (BHN)

24. “Usisahau kuyasifu matendo yake;ambayo watu wameyashangilia.

25. Watu wote wameona aliyofanya Mungu;binadamu huyaona kutoka mbali.

26. Mungu ni mkuu mno hata hatuwezi kumjua;muda wa maisha yake hauchunguziki.

27. Yeye huyavuta kwake maji ya bahari,na kutoka ukungu hufanya matone ya mvua.

28. Huyafanya mawingu yanyeshe mvua,na kuwatiririshia binadamu kwa wingi.

29. Nani ajuaye jinsi mawingu yatandavyo,au jinsi radi ingurumavyo angani kwake?

30. Yeye huutandaza umeme wake kumzunguka,na kuvifunika vilindi vya bahari.

31. Kwa mvua huwalisha watuna kuwapatia chakula kwa wingi.

32. Huukamata umeme kwa mikono yake,kisha hulenga nao shabaha,

33. Radi hutangaza ujio wake Mungu,hata wanyama hujua kwamba anakuja.

Kusoma sura kamili Yobu 36