Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 36:1-13 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Kisha Elihu akaendelea kusema:

2. “Nivumilie kidogo, nami nitakuonesha kitu;maana bado ninacho cha kusema kwa niaba ya Mungu.

3. Nitaleta hekima yangu kutoka mbali sana,na kuonesha kwamba Muumba wangu ni mwadilifu.

4. Kweli maneno yangu si ya uongo;mwenye elimu kamili yuko hapa nawe.

5. “Sikiliza Mungu ni mwenye nguvuwala hamdharau mtu yeyote;uwezo wa akili yake ni mkuu mno!

6. Hawaachi waovu waendelee kuishi;lakini huwapatia wanaodhulumiwa haki zao.

7. Haachi kuwalinda watu waadilifu;huwatawaza, wakatawala na kutukuka.

8. Lakini kama watu wamefungwa minyororo,wamenaswa katika kamba za mateso,

9. Mungu huwaonesha matendo yao maovu,na kwamba wao ni watu wenye kiburi.

10. Huwafungua masikio wasikie mafunzo,na kuwaamuru warudi na kuacha uovu.

11. Wakimtii Mungu na kumtumikia,hufanikiwa katika siku zao zote;miaka yao yote huwa ya furaha.

12. Lakini wasipomtii, huangamia kwa upanga,na kufa kwa kukosa akili.

13. “Wasiomcha Mungu hupenda kukasirika,hawamlilii msaada anapowabana.

Kusoma sura kamili Yobu 36