Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 35:1-10 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Kisha Elihu akaendelea kusema:

2. “Je, Yobu, unaona jambo hili ni sawana kufikiri kinyume cha Mungu

3. ukiuliza: ‘Nimepata faida ganikama sikutenda dhambi?Nimefaidika kuliko kama ningalitenda dhambi?’

4. Mimi nitakujibu wewe,na rafiki zako pia.

5. Hebu zitazame mbingu!Tazama mawingu yaliyo juu kuliko wewe!

6. Ukitenda dhambi, je, Mungu ndiye unayemdhuru?Na kama ukizidisha makosa yako, wadhani unamwumiza?

7. Kama wewe ni mwema, je, unampatia faida,au yeye anapokea kitu kutoka kwako?

8. Uovu wako utamdhuru binadamu kama wewe,wema wako utamfaa binadamu mwenzako.

9. “Kwa sababu ya udhalimu mwingi watu hulia,huomba msaada kwa sababu ya mapigo ya wenye nguvu.

10. Lakini hakuna asemaye, ‘Yuko wapi Mungu, Muumba wangu,mwenye kunifanya niwe mchangamfu usiku,

Kusoma sura kamili Yobu 35