Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 34:9-25 Biblia Habari Njema (BHN)

9. Maana amesema, ‘Mtu hapati faida yoyote,kujisumbua kumpendeza Mungu.’

10. “Kwa hiyo nisikilizeni, enyi wenye ujuzi.Mungu kamwe hawezi kufanya uovu;Mungu Mwenye Nguvu hawezi kufanya kosa.

11. Mungu atamlipa mtu kadiri ya matendo yake,atamlipiza kulingana na mwenendo wake.

12. Ni ukweli mtupu: Mungu hafanyi ovu;Mungu Mwenye Nguvu kamwe hapotoshi haki.

13. Je, kuna aliyemkabidhi mamlaka juu ya dunia?Uwezo wake juu ya ulimwengu ni wake peke yake.

14. Kama Mungu angejifikiria tu yeye mwenyewe,akiondoa pumzi yake ya uhai duniani,

15. viumbe vyote vingeangamia kabisa,naye binadamu angerudi mavumbini.

16. “Kama una akili sikiliza;sikiliza ninachokuambia.

17. Je, anayetawala ulimwengu kwa sheria zake anachukia haki?Je, utathubutu kumhukumu mwadilifu na mwenye nguvu?

18. Amwambiaye mfalme, ‘Wewe ni takataka!’Na watu mashuhuri, ‘Nyinyi ni waovu!’

19. Yeye hawapendelei wakuu,wala kuwajali matajiri kuliko maskini,maana wote hao ni kazi ya mikono yake.

20. Kufumba na kufumbua hao wamekufa;hutikiswa usiku na kuaga dunia;nao wenye nguvu hufutiliwa mbali bila kutumia nguvu za mtu.

21. “Macho ya Mungu huchunguza mienendo ya watu;yeye huziona hatua zao zote.

22. Hakuna weusi wala giza neneambamo watenda maovu waweza kujificha.

23. Mungu hahitaji kumjulisha mtuwakati wa kumleta mbele ya mahakama yake.

24. Huwaangamiza wenye nguvu bila uchunguzi,na kuwaweka wengine mahali pao.

25. Kwa kuwa anayajua matendo yao yote,huwaporomosha usiku wakaangamia.

Kusoma sura kamili Yobu 34