Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 34:4-15 Biblia Habari Njema (BHN)

4. Basi, na tuchague lililo sawa,tuamue miongoni mwetu lililo jema.

5. Basi, Yobu ametamka: ‘Mimi Yobu sina hatia,Mungu ameniondolea haki yangu.

6. Ingawa sina hatia naonekana kuwa mwongo;kidonda changu hakiponyeki ingawa sina kosa.’

7. Ni nani aliye kama Yobuambaye kwake ubaradhuli ni kama kunywa maji?

8. Huandamana na watenda maovuhutembea na watu waovu.

9. Maana amesema, ‘Mtu hapati faida yoyote,kujisumbua kumpendeza Mungu.’

10. “Kwa hiyo nisikilizeni, enyi wenye ujuzi.Mungu kamwe hawezi kufanya uovu;Mungu Mwenye Nguvu hawezi kufanya kosa.

11. Mungu atamlipa mtu kadiri ya matendo yake,atamlipiza kulingana na mwenendo wake.

12. Ni ukweli mtupu: Mungu hafanyi ovu;Mungu Mwenye Nguvu kamwe hapotoshi haki.

13. Je, kuna aliyemkabidhi mamlaka juu ya dunia?Uwezo wake juu ya ulimwengu ni wake peke yake.

14. Kama Mungu angejifikiria tu yeye mwenyewe,akiondoa pumzi yake ya uhai duniani,

15. viumbe vyote vingeangamia kabisa,naye binadamu angerudi mavumbini.

Kusoma sura kamili Yobu 34