Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 34:23-37 Biblia Habari Njema (BHN)

23. Mungu hahitaji kumjulisha mtuwakati wa kumleta mbele ya mahakama yake.

24. Huwaangamiza wenye nguvu bila uchunguzi,na kuwaweka wengine mahali pao.

25. Kwa kuwa anayajua matendo yao yote,huwaporomosha usiku wakaangamia.

26. Huwachapa hadharani kwa ajili ya uovu wao,

27. kwa sababu wameacha kumfuata yeye,wakazipuuza njia zake zote.

28. Hata wakasababisha kilio cha maskini kimfikie Mungu,Mungu akasikiliza kilio chao hao walioteswa.

29. Kama Mungu akinyamaza, nani awezaye kumlaumu?Kama akificha uso wake, nani awezaye kumwona,

30. liwe ni taifa au mtu mmojammoja?Hufanya hivyo, mtu mbaya asitawale,au wale wahatarishao maisha ya watu.

31. “Tuseme mtu amemwambia Mungu,‘Nimekosa, sitatenda dhambi tena.

32. Nioneshe makosa nisiyoweza kuyaonakama nimetenda mabaya sitayarudia tena.’

33. Je, Mungu atapaswa kumwadhibu kama uonavyo wewe?Wewe ndiwe unayeamua, sio mimi.Basi, sema unachofikiri wewe.

34. Mtu yeyote mwenye akili,na kila mwenye hekima anayenisikiliza atasema:

35. ‘Yobu anaongea bila kutumia akili,maneno yake hayana maana.’

36. Laiti Yobu angechunguzwa mpaka mwisho,kwa maana anajibu kama watu waovu.

37. Huongeza uasi juu ya dhambi zake;anaeneza mashaka kati yetu,na kuzidisha maneno yake dhidi ya Mungu.”

Kusoma sura kamili Yobu 34