Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 33:28-33 Biblia Habari Njema (BHN)

28. Mungu aliniokoa nisiangamie Shimoni;nimebaki hai na ninaona mwanga.’

29. “Tazama Mungu humfanyia binadamu haya yote,tena mara mbili, mara tatu.

30. Humwokoa binadamu asiangamie Shimoni,aweze kuona mwanga wa maisha.

31. Sikia Yobu, nisikilize kwa makini;kaa kimya, nami nitasema.

32. Kama una la kusema, nijibu;sema, maana nataka kukuona huna hatia.

33. La sivyo, nyamaza unisikilize,kaa kimya nami nikufunze hekima.”

Kusoma sura kamili Yobu 33