Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 33:26-30 Biblia Habari Njema (BHN)

26. Kisha atamwomba Mungu na kukubaliwa,atakuja mbele yake kwa furaha,na Mungu atamrudishia fahari yake.

27. Atashangilia mbele ya watu na kusema:‘Nilitenda dhambi na kupotosha haki,nami sikuadhibiwa kutokana na hayo.

28. Mungu aliniokoa nisiangamie Shimoni;nimebaki hai na ninaona mwanga.’

29. “Tazama Mungu humfanyia binadamu haya yote,tena mara mbili, mara tatu.

30. Humwokoa binadamu asiangamie Shimoni,aweze kuona mwanga wa maisha.

Kusoma sura kamili Yobu 33