Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 33:2-12 Biblia Habari Njema (BHN)

2. Tazama, nafumbua kinywa changu,naam, ulimi wangu utasema.

3. Nitasema kadiri ya unyofu wa moyo wangu;ninayoyajua nitayasema kwa uaminifu.

4. Roho ya Mungu iliniumba,nayo pumzi ya Mungu Mwenye Nguvu yanipa uhai.

5. Nijibu, kama unaweza.Panga hoja zako vizuri mbele yangu,ushike msimamo wako.

6. Wewe na mimi ni sawa mbele ya Mungu;mimi pia niliumbwa kwa sehemu ya udongo.

7. Kwa hiyo huna sababu ya kuniogopa;maneno yangu mazito hayatakulemea.

8. Kweli umesema, nami nikasikia;nimeyasikia yote uliyosema.

9. Wewe umesema, u safi na wala huna kosa,u safi kabisa na huna hatia;

10. umesema kwamba Mungu anakutafutia kisa,na kukuona kama adui yake.

11. Anakufunga miguu minyororo,na kuchunguza hatua zako zote.

12. “Lakini Yobu, nakuambia hapo umekosea.Mungu ni mkuu kuliko binadamu.

Kusoma sura kamili Yobu 33