Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 33:14-26 Biblia Habari Njema (BHN)

14. Mungu anaposema hutumia njia moja,au njia nyingine lakini mtu hatambui.

15. Mungu huongea na watu katika ndoto na maono,wakati usingizi mzito unapowavamia,

16. wanaposinzia vitandani mwao.Hapo huwafungulia watu masikio yao;huwatia hofu kwa maonyo yake,

17. wapate kuachana na matendo yao mabaya,na kuvunjilia mbali kiburi chao.

18. Hivyo humkinga mtu asiangamie shimoni,maisha yake yasiangamie kwa upanga.

19. “Mungu humrudi mtu kwa maumivu yamwekayo kitandani,maumivu hushika viungo vyake bila kukoma;

20. naye hupoteza hamu yote ya chakula,hata chakula kizuri humtia kinyaa.

21. Mwili wake hukonda hata asitambuliwe,na mifupa yake iliyofichika ikatokeza nje.

22. Yuko karibu sana kuingia kaburini,na maisha yake karibu na wale waletao kifo.

23. Lakini malaika akiwapo karibu naye,mmoja kati ya maelfu ya watetezi wa Mungu,ili kumwonesha lililo jema la kufanya,

24. akamwonea huruma na kumwambia Mungu;‘Mwokoe asiingie Shimoni,ninayo fidia kwa ajili yake.’

25. Hapo mwili wake utaweza kuwa tena kama kijana,ataweza kurudia tena nguvu zake za ujana.

26. Kisha atamwomba Mungu na kukubaliwa,atakuja mbele yake kwa furaha,na Mungu atamrudishia fahari yake.

Kusoma sura kamili Yobu 33