Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 32:6-13 Biblia Habari Njema (BHN)

6. Basi, Elihu mwana wa Barakeli, wa kabila la Buzi akaanza kusema:“Mimi ni kijana, nyinyi ni wazee zaidi;kwa hiyo niliogopa kuwaambieni mawazo yangu.

7. Nilisema moyoni: ‘Waache wenye siku nyingi waseme,wenye miaka mingi wafundishe hekima.’

8. Lakini hiyo roho iliyomo ndani ya mtu,hiyo pumzi ya Mungu Mwenye Nguvu,ndio inayomwezesha mwanadamu kufahamu.

9. Si lazima kuwa mzee ili uwe na hekimawala wazee siyo wenye kufahamu lililo sawa.

10. Kwa hiyo nasema, ‘Nisikilizeni,acheni nami nitoe maoni yangu.’

11. “Basi, mimi nilingojea mlichotaka kusema,nilisikiliza misemo yenu ya hekima,mlipokuwa mnajaribu kutafuta la kusema.

12. Niliwasikiliza kwa makini sana,lakini hakuna mmoja wenu aliyemshinda Yobu;nyote mlishindwa kuyajibu maneno yake.

13. Jihadharini msije mkasema, ‘Sasa tumepata hekima.Atakayemshinda ni Mungu, sio binadamu.’

Kusoma sura kamili Yobu 32