Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 32:11-22 Biblia Habari Njema (BHN)

11. “Basi, mimi nilingojea mlichotaka kusema,nilisikiliza misemo yenu ya hekima,mlipokuwa mnajaribu kutafuta la kusema.

12. Niliwasikiliza kwa makini sana,lakini hakuna mmoja wenu aliyemshinda Yobu;nyote mlishindwa kuyajibu maneno yake.

13. Jihadharini msije mkasema, ‘Sasa tumepata hekima.Atakayemshinda ni Mungu, sio binadamu.’

14. Maneno ya Yobu hayakuwa kwa ajili yangu,kwa hiyo sitamjibu kama mlivyomjibu nyinyi.

15. “Nyinyi mmeduwaa; mmeshindwa,nyinyi hamna cha kusema zaidi.

16. Je, ningoje tu kwa vile hamsemi,kwa sababu mnakaa tu bila kujibu kitu?

17. Mimi pia nitatoa jibu langu;mimi nitatoa pia maoni yangu.

18. Ninayo maneno mengi sana,roho yangu yanisukuma kusema.

19. Moyo wangu umefurika kama divai iliyozibwa,kama kiriba cha divai mpya tayari kupasuka.

20. Ni lazima niseme ili nipate nafuu;yanipasa kufungua kinywa changu na kujibu.

21. Sitampendelea mtu yeyotewala kutumia maneno ya kubembeleza mtu.

22. Maana mimi sijui kubembeleza mtu,la sivyo, Muumba wangu angeniangamiza.

Kusoma sura kamili Yobu 32