Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 30:4-15 Biblia Habari Njema (BHN)

4. Walichuma mimea jangwani na majani msituni wakala,walikula hata mizizi ya mti wa mfagio.

5. Walifukuzwa mbali na watu,watu waliwapigia kelele kama wezi.

6. Iliwapasa kutafuta usalama mapangoni,kwenye mashimo ardhini na miambani.

7. Huko vichakani walilia kama wanyama,walikusanyika pamoja chini ya upupu.

8. Walikuwa wapumbavu wakuu na mabaradhuliambao walilazimika kufukuzwa nchini kwa kiboko.

9. “Na sasa wamenitungia wimbo wa kunizomea,nimekuwa kitu cha dhihaka kwao.

10. Wananichukia na kuniepa;wakiniona tu wanatema mate.

11. Kwa kuwa Mungu amenidhoofisha na kuniaibisha,wamekuwa huru kunitendea wapendavyo.

12. Genge la watu lainuka kunishtakilikitafuta kuniangusha kwa kunitegea.Linanishambulia ili niangamie.

13. Watu hao hukata njia yanguhuchochea balaa yangu,na hapana mtu wa kuwazuia.

14. Wanakuja kama kwenye ufa mkubwa,na baada ya shambulio wanasonga mbele.

15. Hofu kuu imenishika;hadhi yangu imetoweka kama kwa upepo,na ufanisi wangu umepita kama wingu.

Kusoma sura kamili Yobu 30