Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 30:18-31 Biblia Habari Njema (BHN)

18. Mungu amenikaba kwa mavazi yangu,amenibana kama ukosi wa shati langu.

19. Amenibwaga matopeni;nimekuwa kama majivu na mavumbi.

20. Nakulilia, lakini hunijibu,nasimama kuomba lakini hunisikilizi.

21. Umegeuka kuwa mkatili kwangu,wanitesa kwa mkono wako wenye nguvu.

22. Wanitupa katika upepo na kunipeperusha;wanisukasuka huku na huko katika dhoruba kali.

23. Naam! Najua utanipeleka tu kifoni,mahali watakapokutana wote waishio.

24. “Je, mtu akikumbwa na maangamizi hainui mkono?Je, mtu akiwa taabuni haombi msaada

25. Je, sikuwalilia wale waliokuwa na taabu?Je, sikuona uchungu kwa ajili ya maskini?

26. Lakini nilipotazamia mema, mabaya yalinipata,nilipongojea mwanga, giza lilikuja.

27. Moyo wangu wahangaika wala hautulii kamwe;siku za mateso zimekumbana nami.

28. Napitapita nikiomboleza, kwangu hamna jua.Nasimama hadharani kuomba msaada.

29. Kwa kilio nimekuwa ndugu yake mbwamwitu,mimi na mbuni hamna tofauti.

30. Ngozi yangu imebambukamifupa yangu inaungua kwa homa.

31. Kinubi changu kimekuwa cha kufanya matangafilimbi yangu kwa ajili ya kuomboleza.

Kusoma sura kamili Yobu 30