Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 30:11-23 Biblia Habari Njema (BHN)

11. Kwa kuwa Mungu amenidhoofisha na kuniaibisha,wamekuwa huru kunitendea wapendavyo.

12. Genge la watu lainuka kunishtakilikitafuta kuniangusha kwa kunitegea.Linanishambulia ili niangamie.

13. Watu hao hukata njia yanguhuchochea balaa yangu,na hapana mtu wa kuwazuia.

14. Wanakuja kama kwenye ufa mkubwa,na baada ya shambulio wanasonga mbele.

15. Hofu kuu imenishika;hadhi yangu imetoweka kama kwa upepo,na ufanisi wangu umepita kama wingu.

16. “Sasa sina nguvu yoyote nafsini mwangu;siku za mateso zimenikumba.

17. Usiku mifupa yangu yote huuma,maumivu yanayonitafuna hayapoi.

18. Mungu amenikaba kwa mavazi yangu,amenibana kama ukosi wa shati langu.

19. Amenibwaga matopeni;nimekuwa kama majivu na mavumbi.

20. Nakulilia, lakini hunijibu,nasimama kuomba lakini hunisikilizi.

21. Umegeuka kuwa mkatili kwangu,wanitesa kwa mkono wako wenye nguvu.

22. Wanitupa katika upepo na kunipeperusha;wanisukasuka huku na huko katika dhoruba kali.

23. Naam! Najua utanipeleka tu kifoni,mahali watakapokutana wote waishio.

Kusoma sura kamili Yobu 30