Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 29:5-17 Biblia Habari Njema (BHN)

5. Mungu Mwenye Nguvu alikuwa bado pamoja nami,na watoto wangu walinizunguka.

6. Nyakati hizo niliogelea kwenye ufanisi,miamba ilinitiririshia vijito vya mafuta!

7. Nilipokutana na wazee langoni mwa mjina kuchukua nafasi yangu mkutanoni,

8. vijana waliponiona walisimama kando,na wazee walisimama wima kwa heshima.

9. Wakuu waliponiona waliacha kuzungumzawaliweka mikono juu ya midomo kuwataka watu wakae kimya.

10. Sauti za waheshimiwa zilinyamazishwa,na vinywa vyao vikafumbwa.

11. Kila aliyesikia habari zangu alinitakia herina aliponiona, alikubali habari hizo kuwa kweli:

12. Nilimwokoa maskini aliyenililia msaada,kadhalika na yatima asiyekuwa na wa kumsaidia.

13. Waliokuwa karibu kuangamia walinitakia baraka,niliwafanya wajane waone tena furaha moyoni.

14. Uadilifu ulikuwa vazi langu;kutenda haki kulikuwa kama joho na kilemba changu.

15. Kwa vipofu nilikuwa macho ya kuwaonesha njia,kwa viwete nilikuwa miguu yao.

16. Kwa maskini nilikuwa baba yao,nilifanya bidii kutetea haki za watu nisiowajua.

17. Nilizivunja nguvu za watu waovu,nikawafanya wawaachilie mateka wao.

Kusoma sura kamili Yobu 29