Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 29:14-19 Biblia Habari Njema (BHN)

14. Uadilifu ulikuwa vazi langu;kutenda haki kulikuwa kama joho na kilemba changu.

15. Kwa vipofu nilikuwa macho ya kuwaonesha njia,kwa viwete nilikuwa miguu yao.

16. Kwa maskini nilikuwa baba yao,nilifanya bidii kutetea haki za watu nisiowajua.

17. Nilizivunja nguvu za watu waovu,nikawafanya wawaachilie mateka wao.

18. Kisha nikafikiri: Nitafia kiotani mwangu nimetulia;siku za maisha yangu zitaongezeka kama mchanga.

19. Mimi ni kama mti uliotandaza mizizi majini,umande wa usiku huburudisha matawi yangu.

Kusoma sura kamili Yobu 29