Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 29:1-5 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Kisha Yobu akaendelea na hoja yake, akasema:

2. “Laiti ningekuwa kama zamani,wakati ule ambapo Mungu alinichunga;

3. wakati taa yake iliponiangazia kichwani,na kwa mwanga wake nikatembea gizani.

4. Wakati huo nilifikia ukamilifu wa maisha,wakati urafiki wa Mungu ulikaa nyumbani kwangu.

5. Mungu Mwenye Nguvu alikuwa bado pamoja nami,na watoto wangu walinizunguka.

Kusoma sura kamili Yobu 29