Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 28:5-18 Biblia Habari Njema (BHN)

5. Kutoka udongoni chakula hupatikana,lakini chini yake kila kitu huvurugwa kwa moto.

6. Katika mawe yake ndimo vilimo vito vya rangi ya samawatina udongo wake una vumbi la dhahabu.

7. “Njia za kwenda kwenye migodi hiyohakuna ndege mla nyama azijuaye;na wala jicho la tai halijaiona.

8. Wanyama waendao kwa madaha hawajazikanyagawala simba hawajawahi kuzipitia.

9. Binadamu huchimbua miamba migumu kabisa,huichimbua milima na kuiondolea mbali.

10. Hupasua mifereji kati ya majabali,na jicho lake huona vito vya thamani.

11. Huziba chemchemi zisitiririke,na kufichua vitu vilivyofichika.

12. “Lakini hekima itapatikana wapi?Ni mahali gani panapopatikana maarifa?

13. Hakuna mtu ajuaye thamani ya hekima,wala hekima haipatikani nchini mwa walio hai.

14. Vilindi vyasema, ‘Hekima haimo kwetu,’na bahari yasema, ‘Haiko kwangu.’

15. Hekima haiwezi kupatikana kwa dhahabu,wala kwa kupima kiasi kingi cha fedha.

16. Haiwezi kupimwa kwa dhahabu ya Ofiri,wala kwa vito vya Sardoniki au vya rangi ya samawati,

17. dhahabu au kioo havilingani nayo,wala haiwezi kubadilishwa na vito vya dhahabu safi.

18. Hekima ina thamani kuliko matumbawe na marijani,thamani yake yashinda thamani ya lulu.

Kusoma sura kamili Yobu 28