Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 28:1-5 Biblia Habari Njema (BHN)

1. “Hakika kuna machimbo ya fedha,na mahali ambako dhahabu husafishwa.

2. Watu huchimba chuma ardhini,huyeyusha shaba kutoka mawe ya madini.

3. Wachimba migodi huleta taa gizani,huchunguza vina vya ardhina kuchimbua mawe yenye madini gizani.

4. Binadamu huchimba mashimo mbali na makazi ya watu,mbali na watu mahali kusipofikika,wachimba madini huninginia wamefungwa kamba.

5. Kutoka udongoni chakula hupatikana,lakini chini yake kila kitu huvurugwa kwa moto.

Kusoma sura kamili Yobu 28