Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 24:3-15 Biblia Habari Njema (BHN)

3. Huwanyanganya yatima punda wao,humweka rehani ng'ombe wa mjane.

4. Huwasukuma maskini kando ya barabara;maskini wa dunia hujificha mbele yao.

5. Kwa hiyo kama pundamwitumaskini hutafuta chakula jangwaniwapate chochote cha kuwalisha watoto wao.

6. Maskini wanalazimika kuokota mabaki ya mavuno mashambani,wanaokota katika mashamba ya mizabibu ya waovu.

7. Usiku kucha hulala uchi bila nguowakati wa baridi hawana cha kujifunikia.

8. Wamelowa kwa mvua ya milimani,hujibanza miambani kujificha wasilowe.

9. Wapo na wanaowanyakua watoto yatima vifuani mwa mama yao.Wengine huwaweka rehani watoto wa maskini.

10. Watoto hao hufanywa waende uchi bila nguo,wakivuna ngano huku njaa imewabana,

11. wakiwatengenezea waovu mafuta yao,au kukamua divai bila hata kuionja.

12. Kutoka mjini kilio cha wanaokufa chasikika,na walioumizwa hupaza sauti kuomba msaada;lakini Mungu hasikilizi kabisa sala zao.

13. “Wapo wengine waovu wasiopenda mwanga,wasiozifahamu njia za mwanga,na hawapendi kuzishika njia zake.

14. Mwuaji huamka mapema alfajiri,ili kwenda kuwaua maskini na fukara,na usiku ukifika, kazi yake ni kuiba.

15. Mzinifu naye hungojea giza liingie;akisema, ‘Hakuna atakayeniona;’kisha huuficha uso wake kwa nguo.

Kusoma sura kamili Yobu 24