Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 24:19-25 Biblia Habari Njema (BHN)

19. Kama theluji inavyoyeyuka katika joto na ukamendivyo Kuzimu kunavyowanyakua waovu.

20. Maana mzazi wao huwasahau watu hao,hakuna atakayewakumbuka tena.Ndivyo uovu ulivyovunjwa kama mti.

21. “Waovu huwadhulumu wanawake wasiopata watoto.Wala hawawatendei wema wanawake wajane.

22. Mungu, kwa nguvu yake huwaangamiza wenye uwezo,huinuka nao hukata tamaa ya kuishi.

23. Huwaacha waovu wajione salama,lakini macho yake huchunguza mienendo yao.

24. Waovu hufana kwa muda tu, kisha hutoweka,hunyauka na kufifia kama jani,hukatiliwa mbali kama masuke ya ngano.

25. Nani basi, awezaye kuhakikisha kuwa mimi ni mwongona kuonesha kwamba maneno yangu si kweli?”

Kusoma sura kamili Yobu 24