Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 23:1-10 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Kisha Yobu akajibu:

2. “Leo pia lalamiko langu ni chungu.Napata maumivu na kusononeka.

3. Laiti ningejua mahali nitakapompata Mungu!Ningeweza kwenda hata karibu naye.

4. Ningeleta kesi yangu mbele yake,na kumtolea hoja yangu.

5. Ningeweza kujua atakachonijibu,na kuelewa atakachoniambia.

6. Je, angeshindana nami kwa nguvu zake zote?La! Bila shaka angenisikiliza.

7. Yeye aweza kuzungumza na mtu mnyofu,Mungu, hakimu wangu angeamua kuwa sina hatia milele.

8. “Tazama, nakwenda mbele, lakini simpati,narudi nyuma, lakini siwezi kumwona.

9. Namtafuta upande wa kushoto lakini simwoni;nageukia kulia, lakini siwezi kumwona.

10. Lakini yeye anajua njia ninayofuata;atakapomaliza kunijaribunitatoka humo safi kama dhahabu.

Kusoma sura kamili Yobu 23