Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 20:8-17 Biblia Habari Njema (BHN)

8. Atatoweka kama ndoto, asionekane tena,atafutika kama maono ya usiku.

9. Aliyemwona, hatamwona tena,wala pale alipoishi hapatatambuliwa tena.

10. Yeye mwenyewe itambidi kurudisha mali yake yote,watoto wake wataomba huruma kwa maskini.

11. Japo alijisikia amejaa nguvu za ujana,lakini zote zitalala pamoja naye mavumbini.

12. “Mdomoni mwake uovu ni mtamu kama sukari,anauficha chini ya ulimi wake;

13. hataki kabisa kuuachilia,bali anaushikilia kinywani mwake.

14. Lakini ufikapo tumboni huwa mchungu,mkali kama sumu ya nyoka.

15. Mwovu humeza mali haramu na kuitapika;Mungu huitoa tumboni mwake.

16. Anachonyonya mtu mwovu ni sumu ya nyoka;atauawa kwa kuumwa na nyoka.

17. Hataishi kuiona mitiririko ya fanaka,wala vijito vya mafanikio na utajiri.

Kusoma sura kamili Yobu 20