Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 20:4-10 Biblia Habari Njema (BHN)

4. “Wewe labda umesahau jambo hili:Kwamba tangu zamani Mungu alipomuumba mtu duniani,

5. mwovu atajiona ameshinda kwa muda tu,furaha yake asiyemcha Mungu ni ya muda mfupi tu!

6. Mwovu aweza kufana hata kufikia mbingu,kichwa chake kikafika kwenye mawingu,

7. lakini atatupiliwa mbali kama mavi yake.Waliopata kumjua watajiuliza: ‘Yuko wapi?’

8. Atatoweka kama ndoto, asionekane tena,atafutika kama maono ya usiku.

9. Aliyemwona, hatamwona tena,wala pale alipoishi hapatatambuliwa tena.

10. Yeye mwenyewe itambidi kurudisha mali yake yote,watoto wake wataomba huruma kwa maskini.

Kusoma sura kamili Yobu 20