Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 20:16-24 Biblia Habari Njema (BHN)

16. Anachonyonya mtu mwovu ni sumu ya nyoka;atauawa kwa kuumwa na nyoka.

17. Hataishi kuiona mitiririko ya fanaka,wala vijito vya mafanikio na utajiri.

18. Matunda ya jasho lake atayaachilia,hatakuwa na uwezo wa kuyaonja,

19. kwa sababu amewaangamiza maskini na kuwaacha,amenyakua nyumba ambazo hakuzijenga.

20. “Kwa vile ulafi wake hauna mwisho,hataweza kuokoa chochote anachothamini.

21. Baada ya kula hakuacha hata makombo,kwa hiyo fanaka yake yote haitadumu.

22. Kileleni mwa fanaka dhiki itamvamia,balaa itamkumba kwa nguvu zote.

23. Akiwa anajishughulisha kushibisha tumbo,Mungu atamletea ghadhabu yakeimtiririkie kama chakula chake.

24. Labda ataweza kuepa upanga wa chuma,kumbe atachomwa na upanga wa shaba.

Kusoma sura kamili Yobu 20