Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 19:12-21 Biblia Habari Njema (BHN)

12. Majeshi yake yanijia kwa pamoja;yametengeneza njia ya kuja kwangu,yamepiga kambi kuizunguka nyumba yangu.

13. Mungu amewaweka ndugu zangu mbali nami;rafiki zangu wakuu wamenitoroka kabisa.

14. Jamaa zangu na marafiki hawanisaidii tena.

15. Wageni nyumbani mwangu wamenisahau;watumishi wangu wa kike waniona kuwa mgeni.Mimi nimekuwa kwao mtu wasiyemjua.

16. Namwita mtumishi wangu lakini haitikii,ninalazimika kumsihi sana kwa maneno.

17. Nimekuwa kinyaa kwa mke wangu;chukizo kwa ndugu zangu mwenyewe.

18. Hata watoto wadogo hunidharau,mara ninapojitokeza wao hunizomea.

19. “Rafiki zangu wakuu wanachukizwa nami,wale niliokuwa nikiwapenda wamenipa kisogo.

20. Mwili wangu umebakia tu mifupa na ngozi,nimeponea chupuchupu baada ya kupoteza yote.

21. Nioneeni huruma,nioneeni huruma enyi rafiki zangu;maana mkono wa Mungu umenifinya.

Kusoma sura kamili Yobu 19