Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 17:6-9 Biblia Habari Njema (BHN)

6. “Nimefanywa kuwa kichekesho kwa watunimekuwa mtu wa kutemewa mate.

7. Macho yangu yamefifia kwa uchungu;viungo vyangu vyote vimekuwa kama kivuli.

8. Wanyofu wanaduwaa waonapo balaa langu,nao wasio na hatia hujichocheadhidi ya mtu wanayedhani hamchi Mungu.

9. Hata hivyo, mnyofu hushikilia msimamo wake,mtu atendaye mema huzidi kuwa na nguvu zaidi.

Kusoma sura kamili Yobu 17