Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 17:1-6 Biblia Habari Njema (BHN)

1. “Nimevunjika moyo, siku zangu zimekwisha,kaburi langu liko tayari.

2. Kweli wanaonidhihaki wamenizunguka,dhihaka zao naziona dhahiri.

3. “Ee Mungu, uwe mdhamini wangu mbele yako,maana hakuna mwingine wa kunidhamini.

4. Maadamu umezifumba akili za rafiki zangu;usiwaache basi wanishinde.

5. Mtu anayewasaliti rafiki zake kwa faidawatoto wake watakufa macho.

6. “Nimefanywa kuwa kichekesho kwa watunimekuwa mtu wa kutemewa mate.

Kusoma sura kamili Yobu 17