10. Watu wananidhihaki na kunicheka;makundi kwa makundi hunizunguka,na kunipiga makofi mashavuni.
11. Mungu amenitia mikononi mwa wajeuri,na kunitupa mikononi mwa waovu.
12. Nilikuwa nimestarehe, lakini akanivunjavunja,alinikaba shingo na kunipasua vipandevipande;alinifanya shabaha ya mishale yake,
13. akanipiga mishale kutoka kila upande.Amenipasua figo bila huruma,na nyongo yangu akaimwaga chini.
14. Hunivunja na kunipiga tena na tena;hunishambulia kama askari.
15. “Nimejishonea mavazi ya gunia,fahari yangu nimeibwaga mavumbini.
16. Uso wangu ni mwekundu kwa kulia,kope zangu zimekuwa nyeusi ti;
17. ingawa sijafanya dhuluma kwa mkono wangu,na sala zangu kwa Mungu ni safi.
18. “Ewe dunia, usiifunike damu yangu iliyomwagika;kilio changu kienee kila mahali.
19. Nina hakika ninaye shahidi wangu mbinguni,mwenye kunitetea yuko huko juu.
20. Rafiki zangu wanidharau;nabubujika machozi kumwomba Mungu.
21. Laiti mtu angenitetea mbele ya Mungu,kama ifanyikavyo duniani kati za watu wawili.
22. Naam, miaka yangu ni michache,nami nitakwenda huko ambako sitarudi.