Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 15:4-16 Biblia Habari Njema (BHN)

4. Lakini wewe unapuuza uchaji wa Mungu;na kuzuia kutafakari mbele ya Mungu.

5. Uovu wako ndio unaokifundisha kinywa chako,nawe wachagua kusema kama wadanganyifu.

6. Maneno yako mwenyewe yanakuhukumu, sio mimi;matamshi yako yashuhudia dhidi yako.

7. Je, wewe ni mtu wa kwanza kuzaliwa?Je, wewe ulizaliwa kabla ya kuweko vilima?

8. Je, ulipata kuweko katika halmashauri ya Mungu?au, wewe ndiwe peke yako mwenye hekima?

9. Unajua kitu gani tusichokijua sisi?Unafahamu kitu gani tusichokifahamu sisi?

10. Miongoni mwetu wapo wazee wenye hekima,wenye miaka mingi kuliko baba yako.

11. Je, faraja anazokupa Mungu ni ndogo mno?Au je, neno lake la upole kwako si kitu?

12. Mbona moyo unakusukuma kukasirikana kutoa macho makali,

13. hata kumwasi Munguna kusema maneno mabaya kama hayo?

14. Mtu ni nini hata aweze kuwa mwadilifu?au yule aliyezaliwa na mwanamke hata aweze kuwa mwema?

15. Ikiwa Mungu hawaamini hata watakatifu wake,nazo mbingu si safi mbele yake,

16. sembuse binadamu aliye kinyaa na mpotovubinadamu atendaye uovu kama kunywa maji!

Kusoma sura kamili Yobu 15