Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 15:30-35 Biblia Habari Njema (BHN)

30. Hatalikwepa giza la kifo.Ndimi za moto zitakausha chipukizi zake,maua yake yatapeperushwa na upepo.

31. Heri aache kutumainia upuuzi na kujidanganya,maana upuuzi ndio utakaokuwa tuzo lake.

32. Atalipwa kikamilifu kabla ya kufa kwake,na wazawa wake hawatadumu.

33. Atakuwa kama mzabibu unaopukutisha zabibu mbichi,kama mzeituni unaoangusha maua yake.

34. Wote wasiomcha Mungu hawatapata watoto,moto utateketeza mahema ya wala rushwa.

35. Wanatunga udanganyifu na kuzaa uovu.Mioyo yao hupanga udanganyifu.”

Kusoma sura kamili Yobu 15