Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 15:17-33 Biblia Habari Njema (BHN)

17. “Sasa nisikilize, nami nitakuonesha,nitakuambia yale niliyoyaona,

18. mafundisho ya wenye hekima,mambo ambayo wazee wao hawakuyaficha,

19. ambao Mungu aliwapa hiyo nchi peke yao,wala hakuna mgeni aliyepita miongoni mwao.

20. Mwovu atateseka kwa maumivu siku zote,miaka yote waliyopangiwa wakatili.

21. Sauti za vitisho zitampigia kelele masikioni,anapodhani amestawi mwangamizi atamvamia.

22. Mwovu hana tumaini la kutoka gizani;mwisho wake ni kufa kwa upanga.

23. Hutangatanga kutafuta chakula,akisema, ‘Kiko wapi?’Ajua kwamba siku ya giza inamkaribia.

24. Taabu na uchungu, vyamtisha;vyamkabili kama jeshi la mfalme anayeshambulia.

25. Kwa sababu amenyosha mkono wake dhidi ya Mungu;akadiriki kumpinga huyo Mungu mwenye nguvu;

26. alikimbia kwa kiburi kumshambulia,huku ana ngao yenye mafundo makubwa.

27. Uso wake ameunenepesha kwa mafuta,na kiuno chake kimejaa mafuta.

28. Ameishi katika miji iliyoachwa tupu,katika nyumba zisizokaliwa na mtu;nyumba zilizotakiwa ziwe lundo la uharibifu.

29. Mtu huyo kamwe hatakuwa tajiri;wala utajiri wake hautadumu duniani.

30. Hatalikwepa giza la kifo.Ndimi za moto zitakausha chipukizi zake,maua yake yatapeperushwa na upepo.

31. Heri aache kutumainia upuuzi na kujidanganya,maana upuuzi ndio utakaokuwa tuzo lake.

32. Atalipwa kikamilifu kabla ya kufa kwake,na wazawa wake hawatadumu.

33. Atakuwa kama mzabibu unaopukutisha zabibu mbichi,kama mzeituni unaoangusha maua yake.

Kusoma sura kamili Yobu 15