Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 15:14-19 Biblia Habari Njema (BHN)

14. Mtu ni nini hata aweze kuwa mwadilifu?au yule aliyezaliwa na mwanamke hata aweze kuwa mwema?

15. Ikiwa Mungu hawaamini hata watakatifu wake,nazo mbingu si safi mbele yake,

16. sembuse binadamu aliye kinyaa na mpotovubinadamu atendaye uovu kama kunywa maji!

17. “Sasa nisikilize, nami nitakuonesha,nitakuambia yale niliyoyaona,

18. mafundisho ya wenye hekima,mambo ambayo wazee wao hawakuyaficha,

19. ambao Mungu aliwapa hiyo nchi peke yao,wala hakuna mgeni aliyepita miongoni mwao.

Kusoma sura kamili Yobu 15