Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 15:1-11 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Kisha Elifazi, Mtemani, akajibu:

2. “Je, mtu wa hekima hujibu kwa maneno ya upuuzi?Je, mtu huyo amejaa maneno matupu?

3. Je, mwenye hekima hujitetea kwa maneno yasiyofaa,au kwa maneno yasiyo na maana?

4. Lakini wewe unapuuza uchaji wa Mungu;na kuzuia kutafakari mbele ya Mungu.

5. Uovu wako ndio unaokifundisha kinywa chako,nawe wachagua kusema kama wadanganyifu.

6. Maneno yako mwenyewe yanakuhukumu, sio mimi;matamshi yako yashuhudia dhidi yako.

7. Je, wewe ni mtu wa kwanza kuzaliwa?Je, wewe ulizaliwa kabla ya kuweko vilima?

8. Je, ulipata kuweko katika halmashauri ya Mungu?au, wewe ndiwe peke yako mwenye hekima?

9. Unajua kitu gani tusichokijua sisi?Unafahamu kitu gani tusichokifahamu sisi?

10. Miongoni mwetu wapo wazee wenye hekima,wenye miaka mingi kuliko baba yako.

11. Je, faraja anazokupa Mungu ni ndogo mno?Au je, neno lake la upole kwako si kitu?

Kusoma sura kamili Yobu 15