Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 14:11-22 Biblia Habari Njema (BHN)

11. “Kama vile maji yakaukavyo ziwani,na mto unavyokoma kutiririka,

12. ndivyo anavyokufa mtu, wala haamki tena;hataamka tena wala kugutuka,hata hapo mbingu zitakapotoweka.

13. “Laiti ungenificha kuzimu;ungenificha hadi ghadhabu yako ipoe;nao muda ulionipimia ukiisha ungenikumbuka.

14. Je, mtu akifa anaweza kuishi tena?Siku zangu zote za kazi ningekungojahadi wakati wa kufunguliwa ufike.

15. Hapo ungeniita, nami ningeitika,wakati ungetaka kuniona mimi kiumbe chako.

16. Ndipo ungeweza kuzihesabu hatua zangu,ungeacha kuzichunguza dhambi zangu.

17. Makosa yangu yangefungiwa katika mfuko,nawe ungeufunika uovu wangu.

18. “Lakini milima huangukamajabali hungoka mahali pake.

19. Mtiririko wa maji hula miamba,mvua kubwa hufanya mmomonyoko wa ardhi.Ndivyo nawe unavyoharibu tumaini la binadamu.

20. Wewe wamwangusha binadamu, naye akatoweka milele;waubadilisha uso wake na kumtupilia mbali.

21. Watoto wake wakiheshimika, yeye hana habari.Wakiporomoshwa, yeye haoni kabisa.

22. Huhisi tu maumivu ya mwili wake,na kuomboleza tu hali yake mbaya.”

Kusoma sura kamili Yobu 14