Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 14:1-11 Biblia Habari Njema (BHN)

1. “Mtu ni mtoto tu wa mwanamke;huishi siku chache tena zilizojaa taabu.

2. Huchanua kama ua, kisha hunyauka.Hukimbia kama kivuli na kutoweka.

3. Ee Mungu, kwa nini unajali hata kumwangaliana kuanza kuhojiana naye?

4. Nani awezaye kutoa kitu kisafi kutoka kitu kichafu?Hakuna anayeweza.

5. Siku za kuishi binadamu zimepimwa;ee, Mungu umeipanga idadi ya miezi yake;hawezi kupita kikomo ulichomwekea.

6. Angalia pembeni basi, umwache;ili apate kufurahia siku zake kama kibarua.

7. Maana mti ukikatwa lipo tumaini la kuota,waweza kuchipua tena.

8. Japo mizizi yake itazeeka udongoni,na shina lake kufia ardhini,

9. lakini kwa harufu tu ya maji utachipua;utatoa matawi kama chipukizi.

10. Lakini mtu hufa na huo ndio mwisho wake.Akisha toa roho anabakiwa na nini tena?

11. “Kama vile maji yakaukavyo ziwani,na mto unavyokoma kutiririka,

Kusoma sura kamili Yobu 14