Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 13:21-28 Biblia Habari Njema (BHN)

21. Kwanza uniondolee mkono wako unaonipiga,na usiniangamize kwa kitisho chako.

22. “Uanze kutoa hoja yako nami nikujibu.Au mimi nianze, nawe unijibu.

23. Makosa na dhambi zangu ni ngapi?Nijulishe hatia na dhambi yangu.

24. “Mbona unaugeuza uso wako mbali nami?Kwa nini unanitendea kama adui yako?

25. Je, utalitisha jani linalopeperushwa,au kuyakimbiza makapi?

26. Wewe umetoa mashtaka makali dhidi yangu,na kunibebesha dhambi za ujana wangu.

27. Wanifunga minyororo miguuni,wazichungulia hatua zangu zote,na nyayo zangu umeziwekea kikomo.

28. Nami naishia kama mti uliooza,mithili ya vazi lililoliwa na nondo.

Kusoma sura kamili Yobu 13