Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 1:17-22 Biblia Habari Njema (BHN)

17. Huyo naye kabla hajamaliza kusema, mwingine akawasili, akasema, “Wakaldayo walijipanga makundi matatu wakashambulia ngamia, wakawachukua, na kuwaua watumishi wako kwa upanga! Mimi peke yangu nimenusurika ili kuja kukuarifu.”

18. Kabla hajamaliza kusema, akaja mwingine, akasema, “Watoto wako wa kiume na wa kike walikuwa wanakula na kunywa divai nyumbani kwa kaka yao mkubwa.

19. Mara kimbunga kikavuma kutoka jangwani, kikaipiga nyumba hiyo kila upande nayo ikawaangukia, na vijana wote wamekufa, mimi peke yangu nimenusurika ili kuja kukuarifu.”

20. Kisha Yobu akasimama, akararua mavazi yake, akanyoa nywele zake, akajitupa chini na kumwabudu Mungu.

21. Akasema,“Uchi nilikuja duniani,uchi nitaondoka duniani;Mwenyezi-Mungu amenipa,Mwenyezi-Mungu amechukua;litukuzwe jina lake Mwenyezi-Mungu.”

22. Katika mambo haya yote Yobu hakutenda dhambi wala hakumfikiria Mungu kuwa ana kosa.

Kusoma sura kamili Yobu 1